Épisodes

  • Watu wa asili kwenye hatihati ya kutoweka Brazil
    Nov 18 2025
    Shirika lisilo la faida linasema karibu nusu ya jamii za Wenyeji wanaoishi mbali na ulimwengu wanakabiliwa na kutoweka ndani ya muongo kutokana na ukataji miti, uchimbaji wa madini na utalii. Survival International wanasema wanataka ulimwengu - hususan serikali na viwanda - kutambua na kushughulikia tatizo hili kama dharura ya kimataifa.
    Voir plus Voir moins
    8 min
  • Uzalishaji wa Net Zero nchini Australia
    Nov 18 2025
    Muungano umeidhinisha rasmi kuondoa lengo la kutofikia uzalishaji wa gesi chafu katika mkutano wa chumba cha chama huko Canberra. Zaidi ya hayo, Liberals na Nationals wamefunua mpango wa kuondoa mabadiliko ya tabianchi kutoka kwenye orodha ya malengo ya mdhibiti wa nishati ya kitaifa, huku wakiapa kuendelea kupunguza uzalishaji kwa kufuatilia maendeleo ya nchi nyingine.
    Voir plus Voir moins
    8 min
  • Maumivu ya wanawake kutiliwa maanani zaidi
    Nov 14 2025
    Serikali ya Victoria imetoa ripoti ya mwisho ya uchunguzi kuhusiana na uzoefu wa wanawake katika suala la maumivu - na ni taarifa inayosumbua kusoma. kutokana na uzoefu wa wanawake na wasichana 13,000, ripoti hiyo imebaini mapengo katika huduma za afya kwa jinsia, upendeleo katika matibabu, ubaguzi wa kijinsia, na hisia za kupuuzwa au kutopingwa na wataalamu wa afya zinazoenea katika mfumo wa afya wa Victoria.
    Voir plus Voir moins
    8 min
  • Maandamano ya kikundi cha NSN uliwezaje kuruhusiwa kufanyika
    Nov 14 2025
    Maandamano ya neo-Nazi mbele ya bunge la New South Wales yamezua mshtuko katika jamii za Kiyahudi na za tamaduni mbalimbali huko Sydney. Serikali ya jimbo hilo imekashifiwa baada ya kufichuliwa kwamba tukio hilo liliendelea na idhini kutoka kwa Polisi wa New South Wales. Je, ni vipi maandamano haya ya neo-Nazi yalipewa kibali cha kufanyika mwanzoni?
    Voir plus Voir moins
    9 min
  • Mazungumzo kuhusu African Youth Summit 2025
    Nov 14 2025
    Mkutano wa kwanza wa African Youth Summit uliandaliwa na kufanyika mwaka huu, na mratibu wa vijana aliyehudhuria anajiunga nasi kuzungumzia mada ya mkutano huo.
    Voir plus Voir moins
    11 min
  • Idadi ya watoto wa mataifa ya kwanza gerezani yazua tashwishi
    Nov 11 2025
    Serikali ya majimbo na maeneo nchini Australia zitachunguzwa kama sehemu ya uchunguzi wa bunge kuhusu matokeo na athari za kifungo kwa vijana. Kati ya maswala ya kuzingatia katika uchunguzi huu ni Kuzidishwa kwa kufungwa kwa watoto wa Mataifa ya Kwanza.
    Voir plus Voir moins
    9 min
  • Serikali kudhibiti mitandao ya kijamii kuanzia desemba
    Nov 11 2025
    Mtandao wa Reddit na jukwaa la Kick zitaongezwa kwenye majukwaa yanayohitajika kuzuia watumiaji walio na umri chini ya miaka 16, sheria mpya zitakapoanza kutekelezwa mwezi Desemba. Marufuku ya Australia ya mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16, ambayo inajumuisha majukwaa nane kuu, inategemea tathmini zinazoendelea za eSafety ambazo zinaweza kufafanua kati ya huduma za mitandao ya kijamii, ujumbe, na michezo, kuelezea ni kwanini majukwaa kama Steam na Twitch hayakujumuishwa. Wakati serikali ilihakikishiwa na Roblox kwamba wataanzisha teknolojia za kuthibitisha umri ili kupunguza tabia za uwindaji wa watoto, watetezi wa haki za kidigitali wanatahadharisha kwamba marufuku haya yanaweza kuhamasisha watoto kutumia majukwaa madogo yasiyo na uangalizi ambapo wanaweza kukumbana na madhara makubwa zaidi.
    Voir plus Voir moins
    7 min
  • Viza ya milioni moja kutolewa nchini Australia
    Nov 11 2025
    Australia inatarajia kutoa kibali cha kila kudumu ama permanent humanitarian visa , cha milioni moja tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwisho wa mwaka huu. Hatua hii imewezesha sherehe juu ya mchango mkubwa ambao wakimbizi hufanya katika hadithi ya kitaifa ya Australia. Lakini mashirika ya haki za wakimbizi yanasema ni wakati muafaka kufikiria jinsi Australia inaweza kuboresha jibu lake kwa ukimbizi mkubwa wa dunia nzima.
    Voir plus Voir moins
    8 min